Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Mapato Nchini  (TRA)  kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni 1.035   ambayo ni sawa na asilimia 99 .5  ya lengo  kukusanya sh.trioni 1.040 .

Akizungumza   na  waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Bw. Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi  10  wameweza kukusanya sh. Trioni 10.92  ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya sh.trioni 11.02  katika lengo la kipindi hicho.

Amesema kuwa  TRA imedhamiria  kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika  miezi miwili ya kumaliza mwaka wa fedha  ambalo ni sh. Trioni 12.3.

Bw. Kidata amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha  inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo. 

Amesema kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu wowote.

Kamishina Mkuu amesema kuwa wamewakamata wafanyabiashara 300 kwa kuwatoza faini zaidi ya sh. Milioni 746 kwa makosa ya kutotoa risti, kutoa risti zenye bei pungufu pamoja na kutotumia mashine za Kieletroniki  na baadhi yao walihukumiwa kifungo au kulipa faini .

"TRA haitawavumilia wafanyabiashara wanayoikosesha serikali mapato kwa kuuza na kutoa huduma bila risti kwa makusudi yao kamwe hawataachwa", alisisitiza Bw. Kidata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...