Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe wakitoka kukagua nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.



Moja ya nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani. Kaimu Mkurugenzi Mkuu /Mkurugenzi rasilimali Watu na Uendeshaji wa TBC Bi.Joycelin Lugora akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkurugenzi wa wilaya ya Kisarawe (DED) Kisarawe Bi. Mwanamvua Mlindoko na kushoto ni Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBC na Wanahabari wakitoka kujionea hali halisi wakati Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe alipokwenda kukagua nyumba za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.PICHA NA ANNA NKINDA.


Wambura-Sitakubali Rasilimali za Taifa hili zichezewe.

Na.Daudi Manongi-WHUSM

Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.

Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.

“Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.

Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2016

    Miaka yote hii nyumba za shirika walikuwa hawajajipanga vizuri kumalizia hizo nyumba, kuliko kujenga zote zikaishia kwenye linda wangemaliza moja moja. Watafute hela wamamilize hizo nyumba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...