Na Owen Mwandumbya,
Midland Afrika Kusini.
Midland Afrika Kusini.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi kujikita katika umoja na mshikamono.
Mhe. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.
Akizungumzia changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji suluhisho la Pamoja kuyakabili.
“ katika duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo mengi duniani” alisema Ndugai





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...