Baadhi ya watu wanaotaka kusafiri na mabasi ya yaendayo haraka wakiwa katika kituo cha Posta ya Zamani (Baharini) wakipewa maelekezo kuwa katika kituo hicho mashine za kutolea tiketi zimeleta hitilafu kwa leo.
 Basi la mwendo wa haraka likitoka katika kituo cha Posta ya zamani bila kupakia abiria kutokana na kutokuwepo kwa tiketi kwa sababu ya mashine za kituo hicho kuleta hitilafu ya mtandao wa kutolea tiketi.

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
NAULI za usafiri wa Mabasi yaendayo haraka zimeanza kutozwa leo katika jiji la Dar es Salaam huku kukiwa na changamoto nyingi katika vituo vya mabasi hayo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Afisa Uhusiano wa UDART, Deus Bugaywa amesema kuwa changamoto waliokutana nayo ni baadhi ya vituo kukosa mashine za kukatishia tiketi, mafuriko ya watu katika vituo pamoja na chenji kwa wasafiri wanaotumia huduma hiyo.

Amesema mfumo wa kadi ukianza utaondoa changamoto hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam na mfumo wa tiketi utatumika kwa wale ambao wanaingia katika jiji na kuondoka.
Aidha amesema mfumo huo unatakiwa fedha itakayotolewa lazima usome benki kuu kwa kuonyesha kodi katika tiketi, suala la chenji ni chagamoto kutokana na fedha ya chenji waliokuwa nayo ni milioni sita za sarafu lakini zimeweza kuisha.
Baadhi ya wananchi wanaotumia usafiri wamesema kuwa kuanza kwa usafiri huo umekuwa ni mapema kwa kushindwa kuona changamoto hizo.
Mmoja wa wananchi, Juma Said amesema kuwa wamekwenda kukata tiketi katika kituo na kuambiwa waende kituo kinachofuata hali hiyo ameona kuwa ni usumbufu.
Hata hivyo amesema kuwa mtu mmoja anapata tiketi ndani ya dakika 10 ambapo  ni vigumu kwenda na idadi ya watu kuweza kwenda kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2016

    Kama mashine za tiketi zikigoma na ufundi wa haraka hauwezekani kuwepo na plan b ya analogue isiyokuwa digital yaani suluhisho mbadala ili huduma isikwame kwa sababu ya mtandao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2016

    Charira Kibuda, inabidi uandike HITILAFU na siyo HITIRAFU, ops! Ni Chalila.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2016

    km mashine zimekwama wawaruhusu watu kupanda kisha wachajishe nauli kwa mfumo wa kawaida wa daladala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...