TIMU ya Soka ya Uswahilini FC imeibuka mabingwa wa Kombe la Mama Shija baada ya kuichapa Wamangati zote za Mbagala katika fainali ilijaa ushindani mkubwa iliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala Dar es Salaam.

Katika fainali hizo ambazo zilidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Vodacoma, mshambuliaji Sultani Kasikasi wa Uswahilini aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuifungia timu yake mabao 3 yaliyoipatia timu yake ubingwa na kuzawadiwa mpira "hat Trick".

Mabao ya Kasikasi yalipatikana dakika ya 32 , dakika ya 41 na 59 na mabao ya WAmangati yaliyungwa na Salum Gava dakika ya 39 na bao la pili lilifungwa na Musa Madebe aliyeunganisha krosi safi ya Shaaban Pazi.

Muandaaji wa mashindano hayo, Fatuma Shija akizipongeza timu zote 20 zilizoshiriki Kombe hilo aliwataka vijana kutumia muda wao mwingi kwenye michezo ambayo itachukua muda wao mwingi kujenga miili yao badala ya kuvuta bangi na kufanya vitendo vya kihuni mitaani.

Mashindano hayo yalishirikisha timu kuoka Mkuranga mkoa wa Pwani, Wilaya Mpya ya Kigamboni na Temeke, Mshindi wa nne ilikuwa timu ya Kisemvule FC iliyezawadiwa mpira mmoja, mshindi wa tatu ni Bodabdoda iliyopata jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa pili alipata medali 15 za shaba, jezi seti mbili na mpira mmoja.

Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Uswahili baada ya kuzawadiwa Kombe na medali 15 za dhahabu kwa wachezaji wake, jezi seti mbili na mpira mmoja walishangilia na kucheza uwanja mzima huku kuimba nyimbo za ushindi na kuwavutia mashabiki wake na wapita njia.
Muaandaji wa mashindano ya Mama Shija Cup, Fatuma Shija akikabidhi mpira kwa waamuzi wa mashindano yake baada ya kumaliza fainali za Kombe la Shija zilizofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Kingunge, Mbagala na Uswahilini kuibuka mabingwa.
Mwenyekiti wa timu ya Bodaboda ya Mbagala,Ali Omari akipokea jezi seti mbili na mpira mmoja kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilungule baada ya klushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Mama Shija Cup juzi Dar es Salaam.
Mchezaji Sultani Kasikasi wa Uswahilini wa pili kushoto akipongezwa na wenzake kupiga picha na mpira aliozawadiwa baada ya kufunga mabao matatu Hat Trick katika mchezo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...