Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Ronald Lwakatare akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuhusu kuzingatia sheria za barabarani katika kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa na kuepusha ajali.

Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umeonya watuamiaji vyombo vya moto kufuata sheria na kanuni za barabarani ili kurahisisha uendeshaji wa mradi huo na ajali.Wito huu unakuja katika kipindi ambacho mradi huo uko katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa mradi huo katika kipindi cha mpito.

Akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Mhandisi Ronald Lwakatare alisema kutozingatia sheria za barabara za mradi huo, kufikia Ijumaa iliyopita, vyombo vingine vya moto vimesababisha ajali 14 za mabasi ya mradi.

“Ajali hizi zimetokea wakati madereva wa mradi wakiendelea na mazoezi wakijitayarisha na kuanza kipindi cha mpito cha mradi kinachotarajia kuanza hivi karibuni,” alisema.Alisema ajili hizo zimesababishwa na vyombo vingine kuingilia barabara za mradi.Kati ya ajali hizo, tisa zilisababishwa na pikipiki maarufu kama bodaboda, nne zilisababishwa magari na moja ilisababishwa na mwenda kwa miguu.

Alitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kutotumia barabara za mabasi hayo ambazo ni za zege na badala yake kutumia barabara za lami.Pia alisema waendesha bodaboda waache mara moja kutumia vituo vya mabasi ya mradi kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria kwani vituo hivyo si kwa kazi hiyo.

Alifafanua kuwa madereva bodaboda wanapotaka kuvuka kwenye alama za waenda kwa miguu kutoka upande mmoja kwenda mwingine sharti wazizime na kuzikokota na siyo kuziendesha.“Watambue kuwa sheria inawazuia waendesha bodaboda kuvuka pamoja na waenda kwa miguu katika alama hizo huku wakiziendesha,” alionya.

Akizungumzia maandalizi alisema yanakwenda vizuri kwa madereva kuendelea na mazoezi huku wataalamu wengine wakiendelea kukamilisha kufunga mifumo ya utozaji nauli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...