Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu akizindua kujiunga kwa wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) katika huduma ya Bima ya Afya kutoka kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho Askofu Dkt. Rejoyce Ndalima,Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Addo November, Meneja wa NIHF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala na Mwimbaji wa nyimbo za Injili David Nyanda.
 Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu akimkabidhi kadi ya uanacha wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mwimbaji nguli wa muziki wa Injili mzee Makasi mapema wikiendi hii wakati wa hafla ya uzinduzi wampango wa wanachama wa chama cha muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya. Katikati ni Meneja wa NIHF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala na Rais wa CHAMUITA Addo Novemba.
 Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni Constantine Makala akielezea namna wanachama wanavyonufaiki na huduma za mfuko huo mapema wikiendi hii wakati wa hafla ya uzinduzi wampango wa wanachama wa chama cha muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya.
 Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) Addo November akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kujiunga katika huduma ya Bima ya Afya KUTOKA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...