Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

BODI ya Wadhamini ya Timu ya Yanga imetakiwa kuwaarifu wanachama wao juu ya uchaguzi utakaofanyika Mei 27 mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa timu hiyo, Baraka Deusdedit ilisema kuwa utawala wa uongozi wa yanga ulimalizika Julai 14,  2014.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) iliitaka Kamati ya utendaji wa timu hiyo kufuata maadili ya katiba ya Klabu hiyo kutokana na maagizo ya FIFA ya kufanya uchaguzi Juni 30, 2014.

Hata hivyo uongozi wa yanga uliweza kufanya mkutano wa dharula wa wanachama na kushindwa kutimia kwa akidi ya bodi ya wadhamini pamoja na wanachama na kufanya Mwenyekiti na Makamu wake kuendelea na uongozi pamoja na kufanya marekebisho ya katiba ya uongozi huo kuendelea na kazi.

Katika taarifa hiyo ilisema  klabu ya yanga ilitakiwa kufanya uchaguzi katikati ya Mei mwaka jana lakini serikali iliwataka kuahirisha uchaguzi wao na timu hiyo haikuweza kufanya pingamizi hilo  kutokana na kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge pamoja na madiwani.

Timu hiyo katika taarifa yake ilieleza kuwa watafanya uchaguzi kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo na mamlaka yake bila kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maagizo hayo yalitolewa na TFF pamoja na mamlaka za michezo ya kufanya uchaguzi ndani ya siku 33 ambapo kipindi hicho si sahihi kwa klabu ya yanga huku timu yao ikiwa katika mashindano ya Ligi Kuu, Kombe la FA pamoja na  Mashindano ya Kombe la Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...