Kampuni ya simu za mkononi Airtel imetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha inaokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wadogo nchini Tanzania. Airtel imechangia katika kuendesha kampeni ya wazazi Nipendeni (Afya ya wajawazito na Watoto) kwa kutoa elimu kupitia ujumbe mfupi toka mwaka 2012. Mpaka sasa Airtel imeweza kutuma ujumbe mfupi wa taarifa muhimu za afya zaidi ya milioni 22 kwa wateja zaidi ya 350,000 wenye thamani ya shilingi 1,518, 000,000
Airtel kwa kushirikiana na mHealth Tanzania PPP waendeshaji wa huduma hii inayomilikiwa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto inawezesha wateja wake kote nchini kupokea taarifa muhimu za afya ya mama wajawazito na kuwakumbusha kuhudhuria kliniki na kupata chanjo. “Taarifa zinazotolewa kupitia ujumbe mfupi zinahakikisha mtoto ambaye hajazaliwa na mama mjazito wako katika usalama wakati wote” alisema Mratibu na mshauri wa mradi Muttah Saulo kutoka mhealth Tanzania PPP
Aliongeza kwa kusema” akina mama pia wanashauriwa jinsi ya kuwatunza watoto wao kwa usalama baada ya kujifungua, waliojiunga na huduma hii watapata ujumbe mfupi wa idadi isiyopungua nne kwa wiki”
Akiongea kuhusu ushirikiano huo , Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema” Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu wa wazazi nipendeni kupitia huduma yetu ya ujumbe mfupi. Mpango huu unaonyesha uwezo wa teknologia katika jamii na kwamba teknologia ya simu za mkononi inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama. Maelfu ya wajawazito, wazazi na wasaidizi wamenufaika na huduma hii. Kwa kutoa huduma hii bure mpaka sasa tumeweza kuwekeza kiasi cha shilingi 1,518, 000,000 na tunaendelea kushirikiana na mhealth Tanzania PP katika kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu na kuwanufaisha watanzania wengi. Airtel tumejipanga kuendelea kuhamasisha usalama katika maisha ya watanzania na kuwawezesha jamii kufatilia na kutia mkazo katika afya zao kwa kuwapatia elimu juu ya afya bure bila gharama zozote.”
Mmoja kati ya watumiaji wa huduma hii , Bi Francis ambaye sasa ni mama mwenye mtoto wa miezi mitatu alisema” Tunafurahia huu mpango kwani unatupatia elimu juu ya afya zetu na watoto na kutusaidia kufatilia siku za kuhudhuria kliniki pamoja na kuwapeleka watoto kliniki. Mimi na mume wangu tunafurahi huduma hii ya bure kutoka Airtel inayotuwezesha kuendelea kumlea mtoto wetu katika afya.”
Takwimu kutoka katika ripoti ya mHealth Tanzania PPP Mei 2016 zinaonyesha kila mwezi wateja wa Airtel takribani 7300 wamejiunga na huduma ya bure ya sms ya wazazi nipendeni. Kati yao 43% ni wa kina mama wajawazito na 15% ni wa kina mama wenye watoto wadogo na 44% ni wasaidizi wa wakinamama wakiwemo waume , ndugu na wale wanaotafuta taarifa za afya ya uzazi kwa ujumla.
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani ( kulia) na Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans wakipongezana baada ya kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapa taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende”. mradi wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto.
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapatia taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Katikati ni Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi akifatiwa Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans.
Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayo wapatia taarifa mbalimbali za afya ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania na washirika wengine chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Kulia ni Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC)Tanzania, Dr Maestro Evans.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...