KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, BODI YA
MAZIWA TANZANIA INAPENDA KUWATANGAZIA WADAU WAKE
WOTE WA MAZIWA NCHINI WENYE KERO/MAONI / CHANGAMOTO
KUHUSU MASUALA YA UFUGAJI, USINDIKAJI, UKUSANYAJI,
USAMBAZAJI, UINGIZAJI WA MAZIWA NA BIDHAA ZAKE NA WADAU
WOTE WALIOKO KWENYE MNYORORO WA THAMANI WA MAZIWA
KUFIKA OFISI ZA BODI YA MAZIWA ZILIZOPO MIKOCHENI MTAA
WA URSINO NYUMBA NO 13.
VILEVILE KWA WALIO MIKOANI WANAWEZA KUTUMIA TOVUTI YA
BODI, MITANDAO YA KIJAMII, BARUA PEPE AU KUPIGA SIMU
KUWASILISHA MAONI YAO.
BODI ITAPOKEA MAONI HAYO TAREHE 22/06/2016 HADI TAREHE 24/06/2016 KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI HADI SAA 7:00 MCHANA.
BODI ITAPOKEA MAONI HAYO TAREHE 22/06/2016 HADI TAREHE 24/06/2016 KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI HADI SAA 7:00 MCHANA.
IMETOLEWA NA:
NELSON KILONGOZI
KAIMU MSAJILI
BODI YA MAZIWA
Barua pepe: info@tdb.go.tz
Tovuti: www.tdb.go.tz
Simu: +255 22 2771089
+255754 881908
Facebook: tanzaniadairy.board



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...