Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
IKIWA zimesalia wiki moja kuanza kutimua vumbi kwa kombe la Shirikisho Afrika, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) wametoa ratiba ya waamuzi watakaoanza kweny michuano hiyo huku mabingwa wa Tanzania Yanga wakichezeshwa na waamuzi kutoka Morocco dhidi ya wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia na Yanga SC ya Tanzania Juni 19, mwaka huu.

Mchezo huo wa Kundi A utafanyika Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria utachezeshwa na Bouchaib El Ahrach atakayekuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabrouk.

Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa wa Afrika, TP Mazembe Juni 28 katika mchezo wake wa pili wa Kundi A.Kwenye mechi hiyo dhidi ya Mazembe CAF limechanganya waamuzi kutoka nchi tatu tofauti, ambao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O’michael wa Eritrea.

Timu nyingine katika Kundi A ni Medeama ya Ghana ambayo itafungua dimba na TP Mazembe mjini Lubumbashi Juni 17, mwaka huu, mchezo ambao utachezeshwa na waamuzi kutoka Shelisheli Bernard Camille, Hensley Danny Petrousse na Eldrick Adelaide.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...