Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua Dkt. Herbert F. Makoye (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). 
Uteuzi huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa Waziri mamlaka ya kufanya uteuzi huo. Uteuzi huu utaanza tarehe 01/07/2016.
Dkt. Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt. Makoye mwenye Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri - Sanaa (M. A in Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Maonesho.

Imetolewa na,
Genofeva Matemu,
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
28 Juni,2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...