Mkuu
wa
Bidhaa wa benki ya Stanbic Tanzania, Bw Musa Kitoi (kushoto) akiongea
na waandishi wa
habari wakati wa kuchezesha droo ya pili ya kampeni ya miezi mitatu ya
‘weka na
ushinde’’ iliyoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Fundi
magari wa mjini Moshi, Felix
Shirima (43), ameibuka mshindi kwa kupata Sh milioni 3.4. Kulia ni
meneja masoko wa benki hiyo, Evelyn Aguste na afisa wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,
Bw. Jehud Ngolo.
Mkuu wa masoko binafsi wa benki ya Stanbic Tanzania, Lilian Mtali (kushoto) akiongea kwa njia ya simu na Felix Shirima (43), fundi magari mjini Moshi aliyeibuka mshindi wa 3.4m/- baada ya benki hiyo kuchezesha droo ya pili ya kampeni ya miezi mitatu ya ‘weka na ushinde’’ jijini Dar es Salaam jana. Wanaofuatilia kuanzia kulia ni, meneja masoko wa benki hiyo, Evelyn Aguste, afisa wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Jehud Ngolo na mkuu wa bidhaa wa benki hiyo, Musa Kitoi.
Meneja masoko wa benki ya Stanbic Tanzania, Evelyn Aguste (kulia) akichezesha droo ya pili ya kampeni ya miezi mitatu ya ‘weka na ushinde’’ iliyoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Fundi magari wa mjini Moshi, Felix Shirima (43), ameibuka mshindi kwa kupata Sh milioni 3.4. Wanaoshuhudia kuanzia kushoto ni mkuu wa bidhaa wa benki hiyo, Musa Kitoi na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Jehud Ngolo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...