Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dr. Abdallah Possi ( Mb) akizungumza wakati wa majadiliano ya jumla kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu. Mhe. Possi anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tisa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Watu Wenye Ulemavu. Mkutano huu wa siku tatu umeanza siku ya Jumanne hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Wajumbe wengine katika picha ni kutoka kushoto Mhe. Stella Ikupa Alex ( Mb), Mhe. Riziki Said Lulida ( Mb) na Mhe Elly Marko Macha ( MB).
Ujumbe wa Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Mkataba wa Watu Wenye Ulemavu, ufunguzi wa mkutano huu ulifanyika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mkutano huu wa siku tatu ajenda yake ni "Utekelezaji wa Agenda ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030) Kwa Watu Wote Wenye Ulemavu: Pasipo Kumwacha Yeyote”. Unahudhuriwa na Washiriki kutoka nchi 164 ambazo zimeridhia Mkataba huu, Asasi zisizo za kiserikali pia zinahudhuria katika mkutano huu ambao ni maalum kwa watu wenye ulemavu wa aina zote. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...