Na Abel Daud,
Globu ya Jamii, Kigoma.
Globu ya Jamii, Kigoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limemkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamisi Kabatey mwenye umri wa miaka 35 na mkaazi wa kijiji cha Kitahana Wilaya ya Kibondo kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya SMG yenye namba za usajili 1161293 na magazini 01 yenye risasi 23 kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui amesema mtuhumiwa alikutwa kilabuni akitumia pombe za kienyeji baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema. Alipohojiwa mtuhumiwa alikiri kuwa na silaha na kuonesha magazini nyingine ikiwa na risasi 28 na risasi nyingine 51.
Katika mahojiano hayo mtuhumiwa, alitoa siri ya silaha zingine mbili ambazo wenzake walikuwa wametangulia nazo katika eneo la magorofani walipokuwa wamepanga kufanya tukio la utekaji wa magari katika barabara ya Uvinza - Mpanda iliyoko wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Aidha askari polisi wakiwa eneo walipokuwa wamejificha majambazi wengine ghafla walianza kushambuliwa kwa risasi na majambazi hao waliokuwa wamejificha. Katika majibizano hayo licha ya askari kujeruhiwa jambazi mmoja alipigwa risasi bega la kulia na mguu wa kushoto na kufariki wakati akipelekwa hospital.
Hata hivyo majambazi wengine walikimbia baada ya kuzidiwa na mashambulizi ya Askari hali iliyopelekea kupatikana magazine nyingine ya tatu ikiwa na risasi 23 ambapo msako mkali wa kuwasaka bado unaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP Ferdinand Mtui, akionyesha silaha iliyokamatwa kwa mtu huyo
Maafisa wa Polisi Mkoani Kigoma wakijadiliana jambo.
silaha, risasi na magazine zilizopatikana kwenye tukio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...