Kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM redio kinacho tangazwa na Gerald Hando, PJ na Adela Tilya kinachorushwa live kila mwisho wa wiki katika maeneo mbalimbali, leo siku ya Ijumaa ya tarehe 17/06/2016 kimewafikia wakazi wa Kariakoo huku kikiambatana na burudani kabambe kutoka kwa wasanii wa Singeli kama, Sholo Mwamba na Majid Migoma.
Watangazaji wa kipindi cha JOTO LA ASUBUHI, Gerald Hando, PJ na Adela Tilya wakijianda kutangaza live kipindi hicho live.
Mashabiri wa 93.7 Efm Joto la Asubuhi ambao walifika asubuhi na mapema kwa ajili ya kushuhudia kipindi hicho live kutoka Kariakoo.
Msanii Sholo Mwamba akiwaburudisha mashabiki wa Efm redio katika kipindi cha JOTO LA ASUBUHI Kariakoo.
Mashabiki wa Kariakoo wakisikiliza kipindi cha Joto la asubuhi live.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...