Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (katikati) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Chacha Wanyancha (kulia) muda mfupi baada ya kufunga mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali kwa wakufunzi wa Jeshi hilo yaliyofanyika katika kambi ya JKT Mafinga Mkoani Iringa jana. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa. Jumla ya wakufunzi 53 walikabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kulia) na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Chacha Wanyancha wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali kwa wakufunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa yaliyofanyika katika kambi ya JKT Mafinga Mkoani Iringa. Jumla ya wakufunzi 53 walikabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua, (wa tatu kushoto) akimkabidhi Cheti Koplo Agnes Amede baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali kwa wakufunzi wa Jeshi la Kujenga Taifa yaliyofanyika katika kambi ya JKT Mafinga Mkoani Iringa jana. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa, (wan ne kushoto); Mkuu wa Kambi ya JKT Mafinga, Luten Kanali, Hamis Maiga (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mafunzo wa JKT, Kanali Chacha Wanyancha (kushoto). Jumla ya wakufunzi 53 walikabidhiwa vyeti.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...