Mwanamuziki nguli nchini Marekani, Keri Hilson ameingi nchini Nigeria ili kushiriki katika shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika linaloshiriksha nchi 9 barani Afrika ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanadada Melisa John.
Keri Hilson atashirikiana pamoja na majaji wengine katika kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika kwa mwaka 2016. Ambapo Taji la ushindi wa Airtel Trace Music Stars 2015 linashikiriwa na Nalimi Mayunga kutoka Tanzania.
Siku moja baada ya kuwasili , Keri Hilson ameshiriki katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alihainisha kuvutiwa kwake na washiriki na kukiri kwamba bara la Afrika lina vipaji vingi vya muziki na kuwapongeza Airtel na Trace kwa kuanzisha mpango huu wenye lengo la kuinua vipaji na kuwawezesha vijana kuvifikia ndoto zao.
“ naamini finali itakuwa na mvuto sana nimekutana na washiriki na kushuhudia vipaji vya kutosha. Mambo makuu tutakayoangali wakati wa fainali ni pamoja na uwezo wa mshiriki kuweza kutoa burdani , uwezo wa sauti yake na jinsi gani anaweza kutoa burdani kwa mashabiki. Naamini mashindano ya kesho yatakuwa na mvuto nanimejiandaa vyema kufanya kazi na mshiriki atakayeshinda kwa mwaka huu”
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Lagos nchini Nigeria.
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika lagos nchini Nigeria. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Afrika, Dia Ezzaoudi
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha pamoja na Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga
Wafanyakazi wa Airtel kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha pamoja na Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari. Pichani (wa pili kushot) Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania , Bi Jane Matinde
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars, Keri Hilson akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...