Makala Jasper ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika lisilo la kiserikali la Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI).
Juni 16, 2016, alitunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, akiwa ni mshindi miongoni ma washiriki 30 kutoka barani Afrika.Tuzo hiyo imetokana na kazi anayofanya pamoja na wananchi katika Vijiji mbalimbali mkoani Lindi.
MCDI huwezesha wanakijiji kutumia rasilimali za misitu kujenga uchumi na kutunza mazingira. Katika miradi inayofanyika chini ya MCDI, wananchi wameweza kujiendeleza na kujenga shule, hospitali, kununua chakula cha dharura na kutoa misaada kwa vijiji vingine.
Tuzo ya National Geographic Society/Buffet Award ni ya pili kupokelewa na Bw. Jasper. Ya kwanza ilikuwa Whitley Fund for Nature Award aliyopokea nchini Uingiereza tarehe 27 Aprili, 2016. Karibu umsikilize


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...