Hatimaye ile michuano ya kandanda ya nchi za Amerika ya Kusini almaarufu kama 'COPA AMERICA' usiku mwingi wa kuamkia kesho itaingia katika hatua ya robo fainali kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha wenyeji wa michuano hiyo USA dhidi ya EQUADOR ndani ya dimba la Centuary Link Field huko jijini SEATTLE.

Kulingana na wachambuzi wa mambo wanadai kuwa jiji hili ni tofauti kabisa na majiji mengine nchini Marekani kwenye masuala ya mpira wa miguu, wanadai kuwa wenyeji wa jiji hili ni vichaa kweli kweli wa kabumbu na hasa linapokuja suala la timu ya Taifa. Kabla ya mechi watu hukesha wakiwasha mienge na kushangilia kana kwamba mtanange umeisha pigwa na wao wamepata ushindi.
Haya pia amethibitishwa na kocha wa timu hiyo Jurgen Klinsmann "Watu wa Seattle asilimia 1,000 watakuwa nyuma yetu wakitusukuma na kutushangilia, na hilo ni deni kubwa kwetu". Marekani watakuwa wakimtegea zaidi mchezaji Clint Dempsey kuongoza mashambulizi. Swali ni je watavuka kwa nusu fainali?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...