Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati alipokuwa anawasili msibani katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia hizo zilizofiwa katika kitongoji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwapa pole wanafamilia ya marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Nyuma ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo akiwaonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wapili kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (watatu kushoto), nyumba ya kwanza katika Kitongoji cha Kibatini walioivamia watu wanaohofiwa kuwa majambazi na kufanya mauaji. Naibu Waziri na Viongozi hao walienda kutoa pole katika familia zilizofiwa katika Kitongoji hicho kilichopo katika Kata ya Mzizima, mkoani Tanga.
MBARIKIWE SANA VIONGOZI WETU, WANANCHI WATAKUWA WAMEPATA FARAJA SANA KWA KWENDA KUWAONA.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa.
ReplyDeleteNimefurahi kuona serikali inafuatilia jambo hilo kwa makini kwani hii ni vita. Kuchinja raia bila sababu ni jambo la kusikitisha na kuogopesha.
Pamoja na usalama viongozi wa eneo hili muhamasishe na kuchangia maendeleo, picha nilizooona kwenye tv na hapa zinaonyesha huku kunahitaji juhudi za makusudi kupigwe tafu ya kuleta maendeleo na kuinua hali ya maisha ya watu.
ReplyDelete