Michuano ya kandanda ya nchi za Ulaya (EURO 2916) imeingia katika hatua ya robo fainali huku ikishuhudiwa timu zenye majina makubwa na zilizopewa nafasi ya kufanya vizuri au hata kunyakua ubingwa zikitupwa nje ya mashindano, miongoni mwao ni aliyekuwa bingwa mtetezi Hispania, Uingereza na Croatia.
Nchi zilizo fanikiwa kutinga hatua hiyo ya robo fainali ni Poland, Ureno, Wales, Ubelgiji, Ujerumani, Italia, Ufaransa na Iceland au kwa kimatumbi twaweza iita ardhi bafaru. Katika nchi zote hizo Iceland imekuwa ni 'suprise packerg' kwani haikupewa nafasi yoyote lakini imefanya maajabu hasa baada ya kuiondosha Uingereza kwenye hatua ya 16 bora na sasa watapambana na wenyeji siku ya jumapili katika robo fainali ya mwisho.
Robo fainali ya kwanza inaanza kesho Ahamisi, ikizikutanisha Poland na Ureno. Pambano hilo linalotegemewa kuwa kali na la kusisimua litafanyika katika uwanja wa Stade Velodrome, majira ya saa 4 usiku kwa saa za hapa kwetu. Ukiziangalia timu hizi hazitofautiani sana kiushindani kwani katika michezo 10 iliyopita kati yao Ureno wameshinda mara 4, Poland wameshinda mara 3 na wametoka sare mara 3.
Wakati Poland watawategemea zaidi golikipa Lukasz Fabianski, kinda Renarto Sanchez na mzoefu Robert Lewandowski, huku Ureno wao watawategemea Christian Ronald, Luis Nani na mkongwe Ricardo Quaresma, sasa timu ipi itatinga hatua ya nusu fainali? tukutane tena kesho hapa hapa Libenekeni kuendelea kujuzana zaidi na zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...