Katika kusherekea siku maalum ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni, 16 ya kila mwaka, Kamati ya Miss Universe Tanzania kupitia mpango wake mpya uitwao Binti Jasiri ilikutanisha kwa pamoja watoto 90 kutoka vituo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam ambapo halfa hiyo ilihudhuliwa na Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na watoto hao, Makonda aliwambia kuwa serikali ya awamu ya tano inawathamini watoto na hata kuwawekea elimu bure hivyo waongeze juhudi katika masomo yao ili nao waweze kuja kuwa na maisha mazuri na hata kuwasaidia wengine kama jinsi wao wanavyosaidiwa na watu wengine ambao wamefanikiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watoto kutoka vituo mbalimbali vya kulea watoto kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika halfa maalum ya kusherekea siku ya mtoto wa Afrika, Kushoto ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog).

“Watu wenye maisha mazuri wasiwachanganye hata nyie mnaweza kuwa na maisha mazuri hata zaidi yao, mnatakiwa muongeze bidii katika masomo yenu ili na nyie mfanikiwe na kuwasaidia wenzenu kama jinsi mnavyosaidiwa na wengine kwa sasa,” alisema Makonda.

Nae Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot ambaye pamoja na kupata chakula cha pamoja na watoto hao pia alipata nafasi ya kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu maisha, kuwashauri na kuwatia moyo ili waongeze bidii katika masomo yao na hata baadae waweze kufanikiwa kimaisha.

Halfa hiyo ilisimamiwa na Magdalena Gisse na kuhudhuliwa na watoto kutoka Kituo cha Malaika Kids Orphanage, Kurasini Orphanage, Sarafina Orphanage na Makini Orphanage vyote kutoka mkoa wa Dar es Salaam.

Na Rabi Hume, MO Blog
Watoto wakimpigia makofi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza nao katika halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsalimu mmoja wa watoto waliohudhulia halfa maamul ya kumkumbuka mtoto wa Afrika, Aliyembeba mtoto huyo ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na katikati ni Mkurugenzi Kitaifa wa Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...