Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimpa zawadi ya kanga Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo mjini Dodoma.
Picha na Anna Nkinda
Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimwonyesha Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad picha za mazao ya mbogamboga ambayo yamelimwa katika kilimo kinachowezesha mazao mchanganyiko kustawi katika mazingira yenye hali ya hewa iliyodhibitiwa mkoani Mtwara.
Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad akivaa kanga aliyopewa zawadi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura aliyekutana naye leo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Wambura akimwangalia.
Mhe. Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad (kushoto) akimweleza Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na Norway hapa nchini ukiwemo mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia VICOBA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...