Zaidi ya simu 639,000 hadi sasa zimegundulikwa kuwa ni bandia na TCRA wameanza zoezi endelevu la kuzizima moja baada ya ingine usiku huu.Kwa mujibu wa matangazo ya TBC yaliyorushwa live na kuhusisha maofisa wa TCRA wakiwa studio za TBC (juu ) na makao makuu ya TCRA barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam, ilipotimia saa sita na dakika moja simu hizo laki sita zilikuwa zinaendelea kuzimwa.
Dawati la usiku la Globu ya Jamii linaendelea kufuatilia zoezi hili na litatoa updates kila zitapopatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...