Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jamine Tisekwa akiungana na kwaya ya Kikundi cha Sanaa za Maonesho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati burudani ikitolewa bure kwa wananchi katika Bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Sanaa JWTZ ilitoa pia burudani za sarakasi, taarabu, ngoma za asili, Steel Band na muziki wa bendi ya Mwenge Wana Paselepa.

Burudani hiyo ilikonga nyoyo za  wananchi waliofurika kushuhudia ambapo hata muda wa kumaliza ulipowadia hawakutaka watoke eneo hilo.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya kuhusu onesho hilo, alisema kuwa ni jambo ambalo hawakulitegemea hivyo wanaomba tena Sanaa JWTZ wapange siku nyingine waburudishe kuanzia mapema saa nane  hadi jioni ili wananchi wa mkoa huo wafarijike vya kutosha.
Baada ya kumalizi hapo kundi hilo la Sanaa Jwtz lilikwenda kutumbiza usiki kwenye Chuo cha Mipango Dodoma.

Akizungumza Msemaji wa JWTZ SANAA, Hope Dagaa alisema hivi sasa kikundi chao wamekiboresha na kwamba hivi sasa wanataka warudi kwa nguvu zote kwenye kumbi kutoa burudani murwa kwa wananchi, kama ilivyo kuwa zamani.
 Magwiji wa Mwenge Jazz  Wana Paselepa wakifanya vitu vya0.
 Band ya Mwenge Jazz
Taarab na Sarakasi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...