Ndugu Damian Kamugunda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake, Ndugu Longinus  Kamulali Kamunguda, maarufu kwa jina la KK, wa Sinza, Dar es Salaam, kilichotokea alfajiri ya leo, Jumatano, Juni Mosi, mwaka huu, 2016  katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam.

Habari ziwafikie mdogo wake marehemu, Ndugu Venant Karugila na Ndugu Maria Thereza Ludovic wote wa Kijiji cha Kishao , Karagwe, mjomba wake marehemu, Ndugu Clemence Gabriel  wa Kijiji cha Ruzinga, Karagwe na mama yake mdogo marehemu, Ndugu Felister Stephano wa Kiziba, Missenyi – wote wa Mkoa wa Kagera.

Aidha, habari za msiba huo ziwafie ndugu, jamaa na marafiki za familia walioko Mozambique, Canada na Uingereza na wengine wote popote walipo.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu, Sinza Block B, karibu na Lion Hotel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...