Mwenyekiti wa taasisi ya kijamii ya Happy Children Tanzania (HCT) Bi Zainabu Makombe (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya wazi inayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke ikilenga kuhamasisha jamii kupambana na ukatiri dhidi ya watoto. Wengine ni Meneja Masoko msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Mariamu Mwapinga (kulia) na Mwenyekiti wa taasisi ya Glory of Africa ya nchini Sweden Bi.Victoria Lunderberg.

Taasisi ya kijamii ya Happy Children Tanzania (HCT) imeandaa warsha ya wazi inayotarajiwa kufanyika kesho jumamosi ikilenga kuhamasisha jamii kupambana na ukatiri dhidi ya watoto ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliodhimishwa kote barani Afrika hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bi Zainabu Makombe alisema warsha hiyo itakayohusisha baadhi ya taasisi zinazohusiana na utetezi wa haki za watoto itafanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke kuanzia majira saa 3 asubuni hadi saa 7 mchana.

“Ni kwa kushirikiana na wenzetu taasisi ya Glory of Africa ya nchini Sweden tumeweza kuandaa shughuli hii. Tunarajia kwamba shughuli yetu itapambwa na mada mbalimbali za masuala ya afya na haki za watoto zitakazowasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Afya na mashirika kadhaa yanayohusiana namasuala ya watoto hapa nchini,’’ alitaja.

Aidha Bi Makombe alitowa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja hivyo sambamba na watoto wao ili wapate fursa ya kusikikiliza mada muhimu za watoto zitakazoambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Meneja Masoko msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Mariamu Mwapinga ambaye benki ni sehemu ya wadhamini wa warsha hiyo alisema benki hiyo imeamua kushirikiana na taasisi ya HCT kwa kuwa inatambua umuhimu wa watoto na haki zao ndani ya jamii.

“Si tu kwamba tunashirikiana nao katika kufanikisha maadhimisho haya bali pia tutaendelea kuwa nao pamoja katika mipango yao inayokuja kuhusiana na masuala ya watoto na haki zao...Exim tunaamini watoto ni sehemu ya wateja wetu leo na kesho,’’ alisema.

Mbali na Exim baadhi ya taasisi na kampuni zinazoshiriki katika kufanikisha warsha hiyo ni pamoja na Save the Children, PASADA, SOS, White Ribbon, GUTz, Coca Cola, AAR, YWCA na TTO. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...