MSHAMBULIAJI mkongwe wa timu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kuna baadhi ya timu zinahitaji huduma yake ingawa hajataka kuziweka wazi kwani wapo kwenye maongezi na kikubwa zaidi anaangalia maslahi baina yake na timu hizo zinazomuhitaji.

"Nimemaliza mkataba wangu na Simba kwahiyo ni mchezaji huru naweza kujiunga na timu nyingine yoyote ila kwa sasa nipo kwenye maongezi na baadhi ya timu zinazohitaji huduma yangu,"amesema Mgosi. 

Kwa sasa yupo mapumziko baada ya kuwa na majukumu ya kimpira kwa muda mrefu lakini yupo kwenye maongezi na timu itakayoweka dau kubwa atajiunga nao ila ni mapema sana kuzitaja timu hizo.

Mgosi alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa lakini aliweza kukabidhiwa Kitambaa cha kuiongoza timu hiyo kama Nahodha huku katika baadhi ya mechi ambapo kocha Mkuu Jackson Mayanja akitumikia kadi nyekundu na Mgosi  kuchukua majukumu hayo ya kuongoza kikosi cha Simba. 

Hata hivyo Mgosi amekuwa na historia nzuri na wanamsimbazi hao kwani amechezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa sana kabla ya kutimkia katika timu zingine lakini umuhimu wake ulionekana na uongozi kuamua kumrudisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...