Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUFUATIA kutokea kwa vurugu kubwa jana katika mechi yabkimataifa ya kombe la Shirikisho kati ya Yanga na  TP Mazembe na kupelekea kupigwa kwa mabomu ya machozi na kutumika kwa maji ya kuwasha Kamishna msaidizi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke (ACP), Gilles Muroto amesema kuwa jana vikosi vya usalama viliweza kutumia njia hizo kwa ajili ya kutuliza ghasia zilizosababishwa na mashabiki wa mpira waliotaka kuingia ndani na kuzuiliwa kuingia uwanjani.

Akizungumza na Mtandao huu, amesema kuwa walikamata watu takribani watu 20 lakini wameshawaachia kwani walifanya hivyo kwa ajili ya usalama wao na zaidi hawakuwa pale kwa kwa lengo wa kuwakamata bali ni kulinda amani.

"Tulikuwa pale kwa ajili ya kulinda amani na zaidi tuliwakata vijana 20 na tumewaachia tayari kwani tulifanya hivyo kwa kulinda usalama wao kwani vurugu zilikuwa nyingi sana, ila kazi kubwa ilifanywa na vikosi vya usalama na wamefanya kazi kubwa sana,"amesema Muroto. Kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa umeweza kuchukua watu wengi zaidi tofauti na idadi inayohitajika na kwa hali hiyo ilikuwa ni hatari sana pale unapozidisha watu,

Katika mechi hiyo, watu waliweza kujitokeza uwanjani kuanzia majira ya saa 11 alfajiri na kitu kama hicgo hakijawahi kutokea na hata wale mateja pamoja na vibaka walikuwa wengi sana na lazima nguvu ya ziada itumike hasa baada ya wananchi kuvamia geti na kuliangusha na kuanza kuingia ndani kwa nguvu kitu kilichopelekea kuanza kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Uongozi wa Yanga uliwatangazia mashabiki wa soka kuwa hakutakuwa na kiingilio katika mechi yao ambapo maelfu ya watu walikuja kwa wingi na kuweka maswali kwa jamii watu hao wote hawana ajira au waliamua kutokwenda kwenye kazi zao kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo ambayo ilikuwa katikati ya wiki ila hali ya ndani ya uwanja ilikuwa tulivu na amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...