MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa ya kichochezi na si ya kiungwana dhidi ya Rais.
Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa Mbunge Lissu kuripoti katika kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi hilo kuhusu kauli yake aliyoitoa jana baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu kuhusiana na maneno mengine ambayo anayodaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, hivyo atalala huko mpaka kesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...