Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa wito kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.

Wito huo umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

“Mkoa wenu una vivutio vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma ambavyo vikitumika vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .Hata hivyo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo kutatuliwa.

Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.

Aidha alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha katika kila Halmashauri ambapo kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio hivyo. 



Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Hassan Bendeyeko akifungua kikao kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama KinderuKatibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo ya baadhi ya vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Bi. Blantina Raphael wakati alipotembelea makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...