Benjamin Sawe

Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo.

Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.

Aliongezea kuwa walinzi wa kituo hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.

“Tunashangaa hawa walinzi wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.

Nae Bi. Herrieth Shangaa aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kidigitali wa kudhibiti wahalifu.

Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni miundombinu  iliyojengwa kwa  gharama kubwa  sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2016

    Walinzi wawepo, mwanga kwa maana ya taa nazo ziwepo, hata cctv kamera zitamulika wezi na kuwaibua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...