Na Jonas Kamaleki, MAELEZO, Dodoma
10/6/2016
KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni  imemuunga mkono Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha hizo katika miradi ya maendeleo na huduma za jamii kama ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli.
Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya  maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17.
“Tunamuunga mkono Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuondoa posho za vikao (Sitting Allowances) na tunamwomba aondoe posho hizo kwa wabunge nao watumie mishahara yao ili kuwe na usawa,” alisema Silinde.
Silinde alisema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inaunga mkono juhudi za Mhe Rais Magufuli za kukusanya kodi ambayo inabidi ielekezwe kwenye miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.
“Tunaungana na Serikali kukata kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais apanue wigo wa kodi hiyo hadi kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya,” alisema Silinde.
Kwa upande wake, mbunge wa Jimbo la Vunjo (NCCR-Mageuzi), Mhe. James Mbatia amesema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inamuomba Mhe. Rais Magufuli kufuta posho za vikao kwa wabunge haraka ili kuleta usawa kwa watanzania wote.

 Mbunge wa Momba (CHADEMA), Mhe. David Silinde akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Katikati ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Mngwali.
Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi),  Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Kushoto ni Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Mhe. Riziki Mngwali. PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2016

    Kweli ninyi ndio wabunge. Ni waungwana. 2020 mtapata kura nyingi. Juhudi hizi zinalenga kujenga misingi imara ya maendeleoa. Ujenzi wa reli ukianza mama ntilie watapata ajira, simenti itauzwa, vibarua kibao watapata ajira. Hii ndio maana ya kubana matumizi. Na sisi wananchi tunakubaliana nanyi wabunge na Rais wetu. Hizo hela anazobana zinakwenda kuendeleza nchi na si kwenda kutalii nje ya nchi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2016

    The mdudu, asantenii sana hii ni nchi yetu sote so haiingii akilini kupinga kwa kila kitu lazima tushilikiane kwenye mambo muhimu ya nchi yetu ili Tanzania yetu isonge mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2016

    Kweli siasa za njaa tuache. Magufuli anayafanya yale yote wapinzani walikuwa wanayapigia kelele. Sasa wamuunge mkono. Yeye amepiga hatua zaidi. Safari za nje ambazo wapinzani na CCM walikuwa kitu kimoja kuzifaidi sasa zinaleta balaa na malalamishi kutoka hata upinzani. Hebu tuweke maslahi ya nchi na watu wake mbele. Tuache ubinafsi wa posho. Hapa Kazi tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...