MCHAKATO
wa usajili wa washiriki wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016,
umezidi kushika kasi, huku siku tatu zikiwa zimesalia kabla ya
kufanyika kwake Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm
Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa
ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto
wao.
Gidabuday
alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri
chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio
zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100
na mita 50.Alibainisha kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika
Matawi ya Azania Bank popote jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko
Samora Avenue katikati ya jiji.
Aliwataka
wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto wao,
kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na kununua fomu
hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto kushiriki na
kushinda zawadi.Naye, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank
inayodhamini mashindano hayo, Othman Jibrea, alisisitiza umuhimu wa
wazazi na walezi kusajili watoto wao katika Azania Bank Kids Run, ili
kufikia lengo lao la kuibua vipaji vipya vya riadha.
Jibrea
alibainsiha kuwa, Azania Bank imejitosa kudhamini mbio hizo kutokana na
mlengo wake wa kuibua vipaji vichanga katika riadha, hivyo ili kufikia
lengo, wazazui na walezi hawana budi kujitokeza kwa wingi kusajili
watoto wao.Alizitaja zawadi za mbio za Kilomita tano kuwa ni Sh. 200,000
kwa mshindi wa kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000
kwa mshindi wa tatu, wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye
vifaa vya shule na sare za michezo (track suit).
Jibrea
alibainisha kuwa, mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2 atajinyakulia
Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh. 50,000,
pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
Katika
mbio za kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh.
75,000 kwa mshindi wa kwanza, 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000
kwa wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa
vya shule na sare za michezo."Pia, washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio
hizo, watapata kifuta jasho cha Sh. 15,000, begi lenye vifaa vya shule
na sare za michezo. Nia ni kuwafanya watoto watakaoshiriki kutotoka bure
mwishoni mwa mashindano," alisema Jibrea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...