Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Saalam. Katika kikao hicho NIDA iliwasilisha mpango usajili kufikia 31 Desemba 2016 ambapo usajili utakamilika nchini nzima na wananchi kuanza kutumia namba ya utambulisho kupata huduma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed Khamis, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho Ndugu Alphonce Malibiche
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Mifumo ya Komputa (TEHAMA) Ndugu Mohamed Khamis, akifafanua namna mwananchi anaweza kutumia tovuti salama kujua taarifa zake wakati wa kikao na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bi Rose Mdami.

Serikali imekusudia kukamilisha Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote kufikia Desemba 31 mwaka huu.
Akuzungumza na vyombo vya habari leo, msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Rose Mdami, amesema NIDA imepanga kutumia taarifa za NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya Utambulisho kwa wananchi wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA.

Akifafanua, Bi Rose amesema baada ya kuhakikisha kila mwananchi ana Nambari ya Utambulisho, kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili.

“kama mnavyofahamu, katika usajili wa NEC fomu ilikuwa na vipengele 32 vya kujaza kulinganisha na fomu ya NIDA ambayo ina vipengele 74, hivyo ni lazima kila mwananchi kutambua, ili kuwa na utambulisho kamili lazima kujaza vipengele vilivyobaki pamoja na kuambatanisha nakala ya viambata vyake muhimu kuthibitisha taarifa za umri, uraia na makazi” alisisitiza.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...