WAAJIRI waaswa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko Hifadhi ya jamii hapa nchini kwa wakati.

 Hayo yamesemwa na Kamishna wa kazi wa Wizara ya Ofisi ya Waziri  Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu, Hilda Kabisa wakati akizungumza na wanachama wa chama cha waajiri Tanzania jijini Dar es Salaam leo kwenye mkutano wa Mwaka wa Chama cha waajiri Tanzania. 

Amesema kuwa waajiri wengi huwa hawana tabia ya kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati katika mifuko ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha waajiri Tanzania(ATE), Agrey Mulimuka amewaasa waajili kuachana na uwakala wa Rushwa katika nafasi zao wakati wanaajili wafanyakazi katika sehemu zao za kazi.
Pia amesema kuwa waajili waajili wafanyakazi wenye kibali cha ukazi na kuwa na mabadili katika sehemu zao za kazi.
Kamishna wa kazi wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu, Hilda Kabisa akizungumza kwa niaba ya Wizara wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa chama cha waajiri Tanzani (ATE) jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa chama cha waajiri Tanzania, Almas Maige na Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa chama cha waajili Tanzania jijini Dar es Salaam leo. 

Baadhi ya wadau na wa chama cha waajiri Tanzania(ATE) wakisikiliza katika mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...