Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front washerekea siku ya Mtoto wa Afrika na Watoto walipo katika Mahabusu ya watoto iliyopo maeneo ya Regency Hospitali jijini Dar es Salaam leo.

Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika June 16 kila mwaka ambayo ni kumbukumbu ya Watoto wa Afrika kusini walikusanyika pamoja na kuandamana kwaajili ya kudai haki zao hasa haki zao.

Hata hivyo wafanyakazi wa Benki  ya CRDB tawi la Water Front wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliopo katika mahabusu hiyo kwaajili ya mahitaji yao madogo madogo mapoja na kunywa pamoja na watoto hao.
Keki ya watoto wa mahabusu ya watoto  Dar es Saslaam iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front wakikamkabidhi Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan baadhi ya vitu walivyoenda navyo kwaajili ya watoto waliopo katika mahabusu hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water Front akiwa katika picha ya Pamoja na Meneja wa Kituo cha mabusu ya Watoto Dar es Salaam, Ramadhan Hassan jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...