Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA wa ligi kuu Vodacom 2015/2016 Yanga wanatarajia kuondoka siku ya jumapili Juni 12 kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejala utakaopigwa Juni 19 nchini Algeria.

Yanga itaweka kambi nchini Uturuki na itakaa kwa siku chache kabla ya  kuunganisha moja kwa moja nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza na Mo bejan ya Algeria kati ya tarehe 17,18,19 mwezi huu.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa kikosi kitaondoka mapema na kuweka kambi Uturuki ikiwa ni moja ya mikakati ya mwalimu Hans Van De Pluijm katika kujiandaa na mchezo huo wa kwanza na pia kuwajenga kisaikolojia wachezaji hususani kutokana na mechi za ugenini kuwa ngumu sana na fitina pia.

"Timu itaondoka jumapili kuelekea Uturuki na lengo kuu sana ni  kuweza kukiandaa kikosi vizuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mo bejala na tunafahamu utakuwa ni moja ga mechi ngumu sana kwanj tunafahamu tutakuwa ugenini na watatumia mbinu mbalimbali za kututoa mchezoni lakini tunajua jinsi ya kupambana nazo kwahiyo wachezaji watajengwa kisaikolojia na kuweza kutoka na ushindi,"amesema Jerry.

Yanga itaondoka na wachezaji 20 huku Juma Abdul akisalia nchini kutokana na kuwa majeruhi akiumia kifundo cha mguu na nafasi yake kuchukuliwa na Hassan Kessy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...