Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Yanga kinarejea wakati wowote kuanzia kesho kutoka nchini Algeria baada ya kumaliza mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia uliomalizika kwa mabingwa hao wa Ligi kuu Bara kupoteza kwa goli 1-0. Yanga wanakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kufanyika Juni 28 Jijini Dar es salaam ila katika mechi hiyo watamkosa nyota wa kimataifa wa Burundi Amis Tambwe ambaye ampeta kadi mbili za njano.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa wamekubali wamepoteza mchezo huo lakini hawakupendezwa na maamuzi ya mwamuzi wa kati zaidi wanategemwa kufanya vizuri kwenye mchezo unapofuata dhidi ya Mazembe na kwanza watakuwa wapo nyumbani kwahiyo itakuwa ni faida kwao kuondoka na ushindi. “ Tumekubali tumefungwa na zaidi goli halikuwa na matatizo yoyote yale ila tunashukuru kuwa tunajipanga kwa ajili ya mchezo wa pili ambao utakuwa nyumbani dhidi ya Mazembe ni faida kwetu kwani hatutaweza kuruhusu kupoteza katika uwanja wetu,”.

Baada ya kupoteza mchezo huo, kikosi kitarejea nchini kwa ajili ya kujiandaa na wataweka kambi hapa hapa Dar es salaam na kukosekana kwa mchezaji Amisi Tambwe haitakuwa pengo kwao zaidi nafasi yake itachukuliwa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia aliyesajiliwa mapema wiki hii kutoka Fc Platinum ya Zimbabwe, Obrey Chirwa kama usajili wake utapitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). 

Akizungumzia kuhusiana na usajili wa Hassan Kessy ambaye ameshindwa kucheza katika mchezo wa jana dhidi ya Mo Bejaia kwa madai kuwa Klabu ya Yanga walizembea kwenda kuchukua barua kwa Simba na hiyo ndiyo sababu ya kutokuchezea timu hiyo, Muro amesema kuwa wanachokijua wao kuwa Simba hawakutoa barua hiyo na zaidi walifanya hivyo kuwakomoa wao ila watambue kuwa kile lenye mwanzo lina mwisho na ipo siku watakuja kujutia kitendo walichokifanya.

“Tumepata salamu zao kuwa sisi hatukwenda kuchukua barua ya Simba ila ukweli uko wazi kuwa wao ndiyo wametufanyia figisufigisu za kushindwa kutupatia barua hiyo ya kuidhinisha kucheza ila watambue kuwa ipo siku watakuja kujutia kitendo hicho ila siku zote wafahamu kuwa wao wanakimbia lakini njia hawaijui,”amesema Muro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...