Na Zainab Nyamka, Blog ya Jamii

UONGOZI wa Yanga umewasilisha ushahidi wake wa sauti na video katika ofisi za Taasisi ya kudhibiti na kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) kwa ajili ya kuanza kufanyiwa uchunguzi ikiwa ni amri iliyotolewa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji siku aliyochukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo na kuwasikilizisha wanachama wa Yanga sauti za baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), viongozi wa serikali na Mwenyekiti wa matawi Yanga Mohamed Msumi na kumsimamisha uanachama.

Mkuu wa kitengo cha habari, Jerry Muro amesema kuwa hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa na wameshafikisha ushahidi TAKUKURU anachokiamini kuwa watalifanyia uchunguzi na wana uhakika ukweli utawekwa wazi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. "Tumekabidhi ushahidi TAKUKURU na wameupokea na zaidi wamesema kuwa wameupokea na wataufanyia kazi ila hawajasema ni lini uchunguzi utamalizika na kutoa majibu kwa wanayanga wanaotamani haki itendeke na kuona ni jinsi gani viongozi wa mpira hawautendeki haki mchezo huu,"amesema Muro.

Naye Afisa habari wa TAKUKURU, Mussa Msalaba amesema kuwa wamepokea vielelezo vyote ambavyo ni nakala za CD za sauti na video kwahiyo watavipitia na hawawezi kusema uchunguzi utakuwa kwa muda gani ila kesi zote za rushwa huwa zinachukua muda kidogo. Cha msingi tunachowaambia mashabiki na wapenzi wa Yanga kuwa TAKUKURU tunaanza kazi yetu wawe na subira tu kila kitu kitawekwa wazi uchunguzi utakapokamilika.

Yanga wanatarajia kufanya uchaguzi wao Juni 11 wakiwa chini ya kamati ya uchaguzi iliyoundwa na Mwenyekiti Yusuph Manji pamoja na sekretarieti ya Yanga, lakini awali Baraza la Michezo Nchini  BMT liliwataka Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF kusimamia na kuratibu uchaguzi huo kupitia kamati ya uchaguzi wa TFF chini ya Aloyce Komba anayeshukiwa kuwa moja ya wahusika waliokuwa wanataka kuhujumu uchaguzi wa Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...