Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu mzee nae anajichanganya tunajua bila ya ubishi yakwamba ndani ya CCM kuna majipu na sio ndani ya CCM tu bali tunaweza kusema mfumo mzima wa maisha ya mtanzania unaharufu ya jipu. Nnamaana ya kusema yakwamba akitokea mwanafamilia mmoja kuhabatika kupata madaraka serikalini au taasisi yoyote ya umma asipoiba na kujineenesha yeye mwenyewe binafsi kwanza au kuwapatia nafasi za kazi ndugu zake,marafiki na jamaa bila ya kujali sifa stahiki anaonekana mpumbavu. Kinachonishangaza kwa ndugu Lembeli ni kusema aliondoka CCM kwa sababu ndani ya chama hicho kuna mafisadi ndani yake, sikatai hilo kama nilivyokwisha kusema mwanzoni haijalisi awe CCM au Chadema au ukawa watanzania tumekulia kuamini njia ya mkato ili kujipatia kipato ndio njia sahihi wakati ukweli ni kwamba ni mazambi makubwa kuamini hivyo kwani mara nyingi dhana hiyo inatupelekea kutenda vitendo haramu na vile vile dhana ya kutaka kujipatia kipato kwa njia ya mkato ni kiungo sahii cha kutengenezea umasikini,lakini tatizo langu kwa Lambeli kama yeye ni msafi kwanini alimfuata Lowasa? Sio CCM waliomshitaki Lowasa kwa wananchi kuwa ni fisadi bali ni chadema kwa hivyo kwa maana yakwamba mtu anaeangalia mpira jukwaani mara nyingi ndie mwenye kuona udhaifu wa timu pinzani kwa maana hiyo Chadema walikuwa sahihi yakwamba Lowasa ni fisadi.,Sasa kwanini Lambeli alimfuata? Au hizo tuhuma zakwamba Lowasa alikuwa akiwahonga baadhi ya wanachama wenzake maarufu wa CCM ili wamsapoti ni za kweli? Na kama kweli hicho kitu kilitokea ndani ya CCM basi Lambeli yeye mwenyewe binafsi ni hao anaodai mchana ni CCM usiku ni balaa. Nadhani yeye mwenyewe binafsi alikuwa kiongozi wa watu wasiofaa ndani ya CCM. Na kwa mueshimiwa Lowasa kama kweli ni mtu smart/makini basi alipaswa kumjua nani alieiharibu medani yake ya siasa Tanzania lazima atajua yakwamba ni Chadema ndio waliommaliza Lowasa na alifanya makosa makubwa kuchukua maamuzi ya ghadhabu kwenda kujiunga nao. Lowasa hapaswi kuilaumu CCM hata kidogo kwa yote yaliomfika kwani CCM walichokifanya ni kumkata kichwa nyoka aliekwisha kuuliwa. Nilitarajia kumuona mzee lowasa akimjua nani mbaya wake au la sivyo ataendelea kuteseka kwani CCM ni taasisi ngumu kwa vyama vya siasa vilivyopo nchini kwa sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...