Na Zainab Ally Hamis
Dar es salaam School of Journalism(DSJ)
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea majukwaa ya maonyesho Afrika-Karibik, siku ya jumamosi 16 Julai 2016 mjini Bayreuth,Ujerumani pia siku ya 23 Julai 2016 katika tamasha kubwa la International Afrika Festival Tubingen,
siku ya 30 Julai 2016 watatumbuiza XXL Afro Sommer Jam mjini Stuttgart katika Kutur Arena. mzimu huo wa muziki wa bongo dansi utaendelea kudatisha washabiki siku 13 Agosti 2016 mjini Frankfurt katika Afro-Karibik    viwanja vya Robestock Park,Frankfurt,Ujerumani.
Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya imefanikiwa kuwanasa maelfu washabiki kwa wingi inayoongozwa na mwanamuziki nguli  Ebrahim Makunja. a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika maonyesho hayo makubwa na ya aina yake kwa mashabiki wa muziki katika maonyesho hayo, ambapo  watakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band.
Bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Mapenzi ya Pesa" na single CD ya "La Mgambo" pia msikose kusikiliza nyimbo "Supu ya Mawe" ,''Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo zipo katika CD ya "BONGO TAMBARARE" zote zinasikika katika kambi ya FFU au web yao
 Hapo ushindwe wewe tu kuja....
 Kamanda Ras Makunja akiongoza kikosi cha FFU Ughaibuni
 Gwaride la maafande wa kike si mchezo
 Hatumwi mtoto dukani
Nyomi balaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2016

    Kamanda ras makunja mkuu wa ffu na kikosi chake kazi anaimudu nyomi lao la kimataifa ni msimgi tosha

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2016

    Mkuu kuu baba mtakatifu wa Bongo dansi kamanda ras makunja aliyeipindia akili kazi yake,baabu kubwa si mchezo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2016

    Kaka mkuu kamanda ras makunja piga gwaride hakuna kulala mtu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...