Kufuatia tukio la ugeni wa kitaifa wa Mheshimiwa Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India hapa nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), pamoja na Jukwaa la Biashara la India (IBF) na Shirikisho la Biashara na Viwanda la India (FICCI) wanaandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la Kongamano hili ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha wafanyabiashara kutoka katika sekta zifuatazo: Kilimo, Viwanda, Miundombinu, Elimu, Afya, Nishati na Maji.

Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara. Makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi tano za juu kiuwekezaji hapa nchini (kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji). Kulingana na takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kati ya mwaka 1990 na Juni 2016, Kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 2.122.

 Miradi inayoongoza katika kusajiliwa na TIC katika kipindi hicho ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53% ni miradi ya kutoka sekta hii. 

Umma wa wafanyabiashara kutoka Tanzania unakaribishwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia maofisa wafuatao: Ajelandro Sindano (ajelandro.sindano@tic.co.tz/ +255767660777) au Mr. Nestory Kissima (nestory.kissima@tic.co.tz/ +255654075953). Mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni siku ya Jumamosi ya tarehe 9 Julai 2016 saa 6:00 mchana.

Mnakaribishwa sana kushiriki 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...