Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameviagiza viwanda vyote nchini kutumia msibomilia (BARCODES) za Tanzania kama hatua ya kuimarisha masoko na utambulisho wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje ya nchini.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya “NUNUA 620 Nunua Bidhaa za Tanzania” pamoja na Kusherekea miaka MITANO ya Taasisi ya Global Standard One –GSI-kwenye Viwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (SABASABA) mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho.
Makamu wa Rais amesema matumizi ya BARCODES ni muhimu na ni ya lazima kwa sababu yanajumuisha taarifa nyingi ikiwemo asili ya bidhaa,jina la kampuni, kumbukumbu za uzalishaji,utunzaji,usafirishaji na usambazaji wa bidhaa.
Ameleeza kwamba itakuwa ni aibu kubwa kama katika masoko ya ndani ya nchi bado kutakuwa na bidhaa zinazotumia msibomilia (BARCODES) za nje na kusisitiza kuwa matumizi ya Barcodes za Tanzania zitazuia na kupungua upotevu wa ajira kwa wataalamu wa ndani ya nchi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali ya awamu ya TANO ipo Tayari kufanya kazi na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi makubwa yatakayosaidia kukuza uchumi wa Taifa.
Kuhusu uanzishwaji wa Majukwa ya kumwezesha wanawake Kiuchumi nchini, Makamu wa Rais amesema kuwa atahakikisha majukwaa hayo yanaleta matokeo chanya na yenye tija kwa wanawake Wakitanzania mijini na viijijini kwa kuwezeshwa kupata kupata elimu ya ujasiriamali,fursa za masoko,upatikanaji wa mikopo nafuu pamoja na elimu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakwaza wanawake kiuchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizindua kampeni ya NUNUA 620 (msibomilia) katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kushoto) kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango la GS1 mara baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange .
Wanawake kutoka Majukwaa mbali mbali ya Wanawake nchini wakishangilia kwa kujumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wakati maonyesho ya 40 ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...