Na Muhidin Amri,Mbinga

Wilaya ya Mbinga kupitia halmashauri zake mbili za halmashauri ya mji na wilaya, imefanikiwa kukamilisha mradi wa utengenezaji madawati kwa ajili ya kukabiliana na upungufu katika shule za msingi na sekondari wilayani humo.

Kazi hiyo, ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt John Magufuri kwa wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa apa nchini kuhakikisha wanatumia rasimali za maisitu zilizopo katika maeneo yao ili kumaliza tatizo kubwa la madawati lililosababisha baadhi ya watoto waliopo shuleni kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Mkurugenzi mtendaji wa hamashauri ya wilaya ya Mbinga Venance Mwamengo alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili ambapo alifafanua kuwa,wilaya hiyo ilikuiwa na upungufu wa madawati 12,952 kati ya hayo kwa shule za msingi ni 8452 na kwa shule za sekondari kulikuwa na upungufu wa viti na meza 4500.

Hata hivyo alisema, hadi kufikia tarehe 30/6/2016 ambao ni muda wa mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo tayari wamefanikiwa kutengeneza madawati 8000 hivyo kubakia madawati 450 ambayo wanatarajia kukamilisha ndani ya siku tatu zijazo kwa sababu vifaa vyote muhimu kama vile nondo na mbao viko tayari.

Pia Mwamengo alisema, kwa shule za sekondari wamekamilisha kabisa kazi hiyo na kubakiwa na ziada ya viti na meza 1000 ambazo zitasambazwa katika shule za msingi zinazokabiliwa na upungufu ili kumaliaza tatizo hilo la madawati katika wilaya hiyo.

“ apa tayari tumefanikisha kumaliza kazi ya viti na meza kwa shule za sekondari na sasa tunaendelea kumalizia kuunganisha madawati yaliyobaki ambapo ndani ya siku tatu tayari tutakuwa tumeshamaliza kazi yote,hata hivyo hilo sio tatizo kubwa sana kwa sababu tuna ziada ya viti na meza 1000 ambazo tulikusudia kupeleka katika shule za sekondari tutapeleka kwenye shule za msingi ili kufidia upungufu uliopo”alisema Mwamengo.

Kwa mujibu wa Mwamengo ni kwamba wilaya ya Mbinga, ilitenga kiasi cha shilling milioni 475.820 kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati,meza na viti kwa shule za msingi na sekondari hatua akwa kiasif ulani imesaidia kupunguza tatizo hilo.

Mwamengo alisema, kiasi hicho cha fedha ni gharama za kununulia mashine za kuranda,kukata na kukunja vyuma,mashine za kupasulia mbao,umeme, na gharama za zingine ndogo ndogo na yametengenezwa kwa kutumia mbao pamoja na chuma ili kuyafanya yawe imara zaidi ikilinganisha na madawati yanayotengenezwa kwa mbao tupu ambayo uharibika haraka.

Mwamengo alisema, wilaya ya Mbinga ilikuwa na upungufu wa madawati 12,952 ambayo katika shule za msingi upungufu ulikuwa madawati 8,452 na viti na meza kwa shule za sekondari upungufu ulikuwa 4,500,ambapo ilianza kutengeneza madawati mwezi januari mwaka huu na kadri ya agizo hilo walitarajia kukamilisha kazi hiyo tarehe 30 mwezi huu lakini kutokana na changamoto mbalimbali kazi hiyo itakamilika rasmi mwezi huu.
Madawati ya shule ya msingi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma yakisubiri kuunganishwa katika karakana mojawapo inayotumika kwa ajili ya kutengeneza madawati ili kukabiliana na upungufu huo kwa shule za msingi wilayani humo, ambapo wilaya hiyo imefanikiwa kutekeleza kwa asilimia 95 agizo la Rais Dkt John Magufuri.
Baadhi ya meza na viti kwa ajili ya shule za sekondari wilayani Mbinga zikiwa katika karakana ya wilaya hiyo zikisubiri kusambazwa mashuleni ili kumaliza upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari,wilaya ya Mbinga imefanikiwa kumaliza uhaba wa madawati yote 12,850 ambayo yalihitaji kwa shule za msingi na sekondari wilayani humo.
Baadhi ya mafundi wakipandisha madawati kwenye gari kwa ajili kusambaza katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wiayani humo, ambapo wilaya ya Mbinga kupitia halmashauri zake mbili za halmashauri ya mji na wilaya zimefanikiwa kumaliza uhaba wa madawati kwazake, hivyo kuwa wilaya ya kwanza katika mkoa wa Ruvuma kutekeleza kwa asilimia 95 agizo la Rais Dkt John Magufuri alilotoa kwa wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa hapa nchini kuhakikisha wanatumia rasilimali za misitu kumaliza tatizo la upungufu wa madawati.Picha na Muhidin Amri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...