Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Ngabaganga Taraba akifungua mafunzo ya mgambo katika kata za Mwaweja na Ukenyenge wilayani humo, ambapo aliwataka vijana kuwa wazalendo. Akiwapongeza kwa kujitoa kwao kuhudhuria mafunzo hayo, alisema suala la ulinzi wa mali na raia ni la kila mwananchi. Aliwataka kutumia mafunzo hayo kwa mtazamo chanya na kuwa mabalozi wazuri wa amani na uzalendo kwa nchi yao. Aidha, Taraba aliwapongeza wakufunzi wa mafunzo hayo kwa kazi nzuri ya kuwafundisha vijana stadi za ukakamavu ili wawe walinzi wazuri wa amani.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akimkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na vijana wanaopata mafunzo hayo pamoja na watendaji wa vijiji mbalimbali wa kata hizo waliofika viwanjani hapo. Wengine kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Mkuu wa Wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba na kulia ni Afisa kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Yusuf Kambi.
Vijana wanaopitia mafunzo ya mgambo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Ngabaganga Taraba wakati akitoa nasaha zake kwao alipofungua mafunzo hayo kata za Ukenyenge na Mwaweja wilayani humo.
Vijana wakipita kwa ukakamavu mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kishapu, Ngabaganga Taraba pamoja na viongozi mbalimbali walipoonesha namna wanavyopata mafunzo hayo kutoka kwa wakufunzi wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...