Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars" Charles Boniface Mkwasa(Pichani) ameteua kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya kambi maalum ya Taifa Stars kujiandaa na pambano la kukamilisha ratiba ya mbio za kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria.

Vijana wamepewa nafasi kubwa katika kikosi cha Mkwasa huku kiungo wa Mtibwa Sugar Ibrahim Jeba  pamoja na Joseph Mahundi wa Mbeya City na Jamal Mnyate aliyehamia Simba pia wameitwa kwa mara ya kwanza. Mbali na hao pia amemuita kwa mara nyingine tena Saimon Msuva na Oscar Joshua.

Timu hiyo itaingia kambini Agosti 1 hadi 5 ikiwa ni kambi ha awali kwa ajilo ya kuwaweka sawa kisaikolojia huku kati ya Agosti 23-25 wataingia kambi ya mwisho kabla ya kuondoka kwa ajili ya kwenda kuwavaa katika mchezo wa marudiano Septemba 02.

Kikosi Kamili:
Walinda Milango: Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benno Kakolanya.

Walinzi: Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Mohamed Hussein, Juma Abdul, Erasto Nyoni.

Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Hassan Kabunda, Simon Msuva.

Washambuliaji: Joseph Makundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Hajib, John Bocco, Jeremiah Juma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...