Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sostenes Lyimo, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godious Kahyarara, na wasaidizi wake wakati walipotembelea katika Banda la Maonesho la Mfuko huo kwenye Viwanja vya Sabasaba jana. Picha na Mafoto Blog
Afisa Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janeth Ezekiel, akizungumza na mwananchi aliyefika kwenye Banda lao la Maonesho katika Viwanja vya Sabasaba wakati akimwelekeza jambo kuhusu mafao ya Mfuko huo.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godious Kahyarara (katikati) walipokuwa wakitembelea Banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Sabsaba.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Saluna Aziz Ally (kulia) na Glory Maboya, wakiendelea kutoa huduma kwa wateja wao waliofika katika Banda la maonesho Sabasaba la mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio akihojiwa na Waandishi wa habari baada ya Mfuko wake kukabidhiwa Kikombe cha ushindi wa kwanza wa Kundi la Mifuko ya Hifadhi ya jamii na Makampuni ya Bima katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...