Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.

Warembo walioingia tano bora. Kutoka kulia ni Catherine Listone, Sia Pius, Hafsa Mahamood, Saida Khalifa na Faith Msuya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano hilo kitita cha sh.500,000.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabishi mshindi huyo moja ya katoni ya windhoek kati ya tano zilizotolewa na kampuni hiyo kwa mshindi huyo ambapo pia mshindi wa pili na watatu walikabidhiwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Sinza 2016 imemtangaza Sia Pius kuwa mshindi wa Windhoek Draught Miss Sinza 2016 baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Defrance iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana usiku.

Pius aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake tisa waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Catherine Listoni huku ya tatu ikichukuliwa na Hafsa Mahamood.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spiritis kupitia bia ya Windhoek pamoja na wadhamini wengine.Mshindi wa kwanza wa shindano hilo alizawadiwa sh.500,000 wakati wa pili akijipatia sh.300,000 na watatu akiondoka na kitita cha sh.200,000 huku washiriki wengine wakiondoka na kifuta jasho cha sh.100,000 kila mmoja.

Washindi hao watatu wataingia moja kwa moja katika shindano la kumsaka Miss Kinondoni 2016 litakalofanyika mwezi ujao.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...